Home

Monday, August 1, 2011

GAMBA, MRITHI WA ROSTAM ZAWA AJENDA MOTO

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa na katibu mkuu wa chama hicho. Willson Mukama (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzannia Zanzibar, Aman Abeid Karume wakati wa ufunguzi wa kamati kuu ya chama hicho mjini Dododoma juzi.
KAMATI Kuu ya CCM, (CC) jana ilikutana mjini Dodoma huku  mpango mkakati wa kujivua gamba na uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga mkoani Tabora, zikiwa ni agenda moto katika kikao hicho kilichoketi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.Mkutano huo wa CC umefanyika kipindi ambacho chama hicho tawala, kimepigwa na mawimbi mazito ya kisiasa kutokana na mpango huo wa kujivua gamba, ambao unaungwa mkono na baadhi ya makada wa chama hicho huku wengine wakipinga jinsi unavyotekelezwa.

No comments:

Post a Comment