
Msanii Ludacris kutoka nchini Marekani na ambaye anasubiriwa kwa hamu kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki hususani wa Hip Hop/Rap,asubuhi hii ameweka wazi mbele ya waandishi wa habari kwamba yupo tayari kabisa kuwapa mashabiki hao burudani ya kipekee na ya aina yake wakati atakapopanda jukwaani hapo kesho katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar-es-salaaam.Ludacris ambaye alizaliwa huko Champaign,Illinois 11 mwezi September mwaka 1977 ameweka wazi kwamba anazo nyimbo za kutosha kabisa ili kuwapagaisha wapenzi wa muziki.Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyikia katika hotel ya Kempinsk Kilimanjaro jijini Dar,Ludacris alionekana mchangamfu na mtu anayejiamini kabisa kwa kitu anachotarajia kufanya hapo kesho. Kazi kwako mpenzi wa fiesta
No comments:
Post a Comment