Home

Saturday, July 30, 2011

Kocha Sounders: Amwambi Ngassa ajifunze kukakaba

Pamoja na kufanya vizuri kwenye majaribio na kufuzu kocha, Sigi Schmid wa Seattle Sounders amemtaka mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Azam, Mrisho Ngassa kujifunza kusaidia ukabaji.
Ngasa amepewa na timu hiyo ya Sounders nafasi ya pili ya kurudi tena Marekani na kujiunga nayo hapo mwezi  Februari mwakani wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha dogo Amerika Kaskazini.“Unapokwenda sehemu kama Tanzania na unapomuona mtu mmoja aliyesimama juu ya mabega ya wenzake wote, utajaribu kujiuliza kwanini imekuwa hivyo,” alisema Schmid.
Jibu la haraka ni Ngassa pekee.Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 5, anawezza kutumia kasi yake na ujanja wa kupenya mabeki na kutengeneza nafasi.  Hata dhidi ya Manchester United aliweza kutumia nafasi ndogo aliyopata kupiga shuti lililopaa kwa kuiba mpira mbele ya beki  Rio Ferdinand.“Ngasa si mchezaji mkubwa, lakini nina uzoefu ya wachezaji wafupi kufanya vizuri hapa Seattle, hivyo sio jambo litalotusumbua.  Ni mchezaji mwenye kasi.  Nafikiri kasi yake akiwa kwenye eneo fupi ni kitu cha kipekee,” alisema Schmid. “Kiufundi, ni mzuri.  Anaweza kukokota mpira na kupiga mashuti vizuri.  Anaweza kusoma mchezo vizuri.  Nafikiri anahitaji kujirekebisha kwenye ulinzi zaidi, lakini ni mchezaji mzuri kwenye kushambulia na mwepesi wa kuzoeana na wenzake uwanjani hilo ni jambo zuri,” alisisitiza Schmid.Kauli hiyo ya kocha wa Sounders inaungana na ile ya mwenzake wa Taifa Stars, Jan Poulsen aliyewahi kusema Ngasa anatakiwa kujifunza kukaba kama soka ya sasa inavyotaka ili aweze kuwa mchezaji aliyetimia.Kusajiliwa kwa Ngassa na timu  hiyo inayoshiriki  ligi kuu ya Marekani kumekuja baada ya kufuzu majaribio aliyoyafanya katika kikosi hicho  kwa takribani mwezi mmoja.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Azam, Nasoro Idrisa alisema taarifa zilizowasilishwa kwao na kocha wa Seattle,  Schmid, Ngasa alifanikiwa kufuzu majaribio yake ambapo ameruhusiwa kurejea nyumbani na kutakiwa kurudi nchini humo kwa ajili ya kusajiliwa  rasmi wakati wa usajili wa dirisha dogo ambao hufanyika Februari."Kimsingi tulikuwa tunawasiliana na kocha wa Seattle  muda wote wa majaribio ya Ngasa, lakini jambo zuri ni kwamba  alitupa taarifa ya Ngasa kufanikiwa katika majaribio na sasa anatakiwa kurejea nchini humo kwaajili ya kusajiliwa rasmi mwezi Februari wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha dogo."Tunamtarajia atatua nchini leo na kuendelea na majukumu katika klabu yake kama kawaida na hivyo ndivyo tulivyokubaliana toka awali,"alisema Idrisa.Aliongeza kuwa kwa upande wao hakuna kikwazo ambacho kinaweza kumzuia  Ngasa kutimiza ndoto zake na klabu yake akisema anaamini pande zote zitaafikiana katika suala la kiwango cha fedha za mauzo ya nyota huyo."Jambo muhimu kwanza tunashukuru amefanikiwa na ndio kitu muhimu kwani suala la makubaliano katika bei ya kumuuza sidhani kama ni tatizo, naamini pande zote mbili zitaafikiana,"alisema Idrisa.Baraza la vyama vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limewataka wachezaji wa ukanda huu kuiga na kufuata nyayo za mchezaji  Mrisho Ngassa  ambaye hivi karibuni aliweka historia kwa kuchezea timu ya Seattle Sounders ya Marekani dhidi ya Manchester United ya England.Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema kuwa bidii aliyoonyesha Ngassa ni mfano wa kuigwa kwani ameweza kucheza mechi dhidi ya timu bora duniani huku akiwa hajasaini fomu yoyote ya usajili.Musonye alisema kuwa hatua ya Ngassa kucheza mechi hiyo ni faraja kwa Tanzania na ukanda wa soka wa Afrika Mashariki na Kati kwani ndiyo kanda pekee katika bara la Afrika linaloshindwa kufanya vyema katika mashindano mbali mbali.Alisema Ngasa ni miongoni mwa wachezaji nyota kama Macdonald Maliga na Denis Oliech ambao wanacheza Italia na Ufaransa wakati Ukanda huu una wachezaji wengi ambao wana uwezo wa kufanya vyema, lakini wanashindwa kutokana na kukosa ari ya kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment